Xhaka ataka kurudi Bundesliga

0
74

LONDON, England

KIUNGO wa Arsenal, Granit Xhaka, anavutiwa na mpango wa kurejea katika klabu yake ya zamani ya Borussia Monchengladbach.

Lakini, Xhaka raia wa Uswis mwenye umri wa miaka 26, anataka hilo litokee pale atakapomaliza mkataba wake na Arsenal mwaka 2024. 

Nyota huyo amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Washika Bunduki tangu aliposajiliwa mwaka 2016, ambapo ameshashuka dimbani mara 225.

Hata hivyo, kiwango chake kimekuwa kikishuka mara kadhaa na itakumbukwa alikaribia kuuzwa mwaka jana, kabla ya kupewa mkataba wa miaka mitatu.

Source: mtanzania.co.tz